WELCOME TO ANNAPITA.COM

For more entertainment News

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa

WASANII WA MUZIKI TANZANIA

Keep you informed always

TANZANIA BONGO ARTISTS

Annapita Ukutani

WELCOME TO ANNA PETER OFFICIAL WEBSITE

Kwa habari Za Burudani na zenye uhakika.

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Annapita Ukutani

Sunday, March 1, 2015

Wasanii Wakike na Watangazaji Washiriki Kwenye Video ya Kampeni 'Simama Nami'

Madam Ritha, Kajala, Mtangazaji Dida,Shadee,Sauda Mwilima,Zamaradi,Shilole,Mwasiti na mimi mwenyewe ni baadhi ya watu maarufu wa kike kutoka sekta mbalimbali waliojitokeza kumuunga mkono msanii Keisha katika utengenezaji wa video ya wimbo wa 'Simama Nami'.Wimbo huo unabeba jina la Kampeni yake ambayo inahamasisha jamii kuacha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Msanii Keisha 
Shughuli ilianza kea make up kwa wasanii hao ambapo Diana wa American Nails ndo alikuwa anasimamia mpango huo kuhakikisha kila mtu atakayeonekana anapendeza.
Mimi,Grace Matata na Princess
Princess na Queen Darleen
Mwasiti na Princess
Keisha alisema Wimbo wa 'Simama Nami' ni awamu ya kwanza ya kampeni hiyo.Kwani amesema anaona kama Serikali haiko seriuz na swala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo ameamua kujitoa ili kuwatetea wenzake

Thursday, January 22, 2015

KILIMO KINALIPA - MAKALA

Niko mtaa ambao ni maarufu kama mtaa wa Anna Makinda eneo ambalo Mh Spika wa Tanzania Anna Makinda anaishi,Kijitonyama Mabatini Polisi .Ni eneo ambalo nimekutana na mama ambaye kipato chake ni kuanzia laki 4 hadi 8 kwa mwezi kutokana na kilimo cha mbogamboga.Hakika ’kilimo kinalipa’.
Monica Mlowe.
Monica Mlowe ni mama wa watoto wawili ambaye anajishughulisha na kilimo cha mbogamboga hapa jijini Dar es salaam kwa miaka 19 sasa.Monica aliamua kilimo iwe njia yake ya kujiingizia kipato cha kukidhi mahitaji yake yakila siku pamoja na familia yake baada ya kupunguzwa kazi.Mama huyo  anasema kuwa alikuwa ameajiriwa kama Katibu Muhtasi katika moja ya shirikika la Umma hapa nchini.Alifanya kazi katika shirika hilo kuanzia mwaka 1979 hadi mwaka 1996.
Mama huyo anaendelea kueleza kuwa alichagua kilimo kwasababu tangu akiwa nyumbani kwa wazazi wake huko Dodoma alikuwa anapenda kilimo na ndiko alikojifunza kilimo.Monica anasema mwaka 1996 alienda Kariakoo katika maduka yanayouza mbegu na shilinig 2000 ambako alinunua mbegu za mchicha za 500, majani ya kunde za 500, majani ya maboga za 500 pamoja na mbegu za matembele za 500. “Kwakweli nilianza na mtaji mdogo tu nikarudi nyumbani nikatengeneza eneo vizuri kwasababu palikuwa hapajawahi kulimwa kabsaa nikaanza kulima”, Monica.
Baada ya mboga kukua alianza kupita katika nyumba za majirani nakuwaambia kuwa anauza mboga nyumbani kwake.Monica alianza kupata wateja majirani zake na baada ya wigo wa biashara yake kukua alianza kupata wateja wafanyabiashara wanaotembeza bararani ambao wananunua kwake kwa bei ya jumla.
Hivisasa Monica anauza mboga kuanzia shilingi 1000 kwa bei ya rejareja, moja ya wateja wakubwa ni pamoja na Mh Anna Makinda Spika wa bunge la Tanzania ambaye kwa mujibu Bi Monica ni mteja wake wa mboga kuanzia mwaka 1998.
Mama Abdul ni moja ya wateja wake ambaye wakati nafanya mahojiano na Monica alikuja kununua mboga.Mteja huyo alisema anapenda kununua mboga hapo kwa sababu anajua zinalimwaje,hatumii madawa na ni jirani yake.
Monica alisisitizia kuhusu usalama wa mboga kuwa ni kweli yeye hatumii mbolea zenye kemikali, “mimi natumia mbolea ya kuku, maji ninayomwagilia ni masafi kabsaa,nimechimba kisima hapa,kwahiyo maji yakumwagilia nachota kwenye kisima”, alieleza.
Kwa miaka 19 sasa Monica ameweza kusomesha watoto wake wawili mpaka elimu ya chuo kikuu.Alisema kuwa mtoto wake wa kwanza Happyness Mlewa alisoma masomo ya uandishi habari na hivisasa ni mtangazaji wa redio Maria.Pia mtoto wake wa pili anayeitwa John Mlewa amemaliza stashada katika chuo kikuu cha Dodoma mwaka jana.Nilizungumza na mtoto huyo ambaye alinambia kuwa japo hakuwa na mkopo wa serikali wa elimu ya juu lakini hakuwahi kupungiwa na kitu chochote.John aliendelea kusema kuwa uthubutu wa mama ake umemfanya yeye kujiamini kuwa mtu unaweza ukafanya kitu chochote ukiamua na ukafanikiwa.
Mkulima huyo alisema changamoto anazokabiliana ni katika mbegu ambapo wakati mwingine hununua mbegu zilizokaa muda  mrefu bila kujua.Monica anasema mbegu zilizokaa kwamuda huwa zinasumbua kuota kwahiyo unakuta ni hasara kwake.Changamoto nyingine alieleza kuwa ni upatikanaji wa mbolea ya kuku ambao kwasasa ni adimu.
Monica aliiasa jamii haswa wanaoishi mijini kuwa na bustani ndogo za mboga kwaajili ya familia na si kutapanda maua tu peke yake.Ameshauri hata watu wanaofanya kazi haswa wanawake kuwa wanaweza wakafanya shughuli za kilimo kama njia ya ziada ya kujiingizia kipato.
Mpaka hapo utakubaliana na mimi kuwa kilimo kinalipa, na hii ndo maana huu usemi uko Tanzania kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu.Hii ni sehemu ya kwanza ya makala hii ya 'Kilimo Kinalipa'.Usikose kusoma sehemu ya pili ujue tutakuwa na mkulima gani.

SHAA ATOA USHAURI KWA WASANII WAKIKE

Sarah Kaisi maarufu kama Shaa amesema kuwa wasanii wakike Tanzania inabidi wachukulie muziki kama kazi ili waweze kufata mafanikio zaidi.
Msanii huyo ambaye mwaka jana alifanya vizuri na wimbo wa 'Subira' 'Njoo' ambayo alifanya colabo yake ya kwanza na msanii mkubwa wa Kenya Redsan alisema kuwa mwaka jana aliweza kuingiza pesa zaidi kuliko miaka yote tangu aanze muziki.Shaa aliendelea kueleza kuwa kilichomuwezesha yeye kufanya shoo kubwa, kupata dili ya Coca popstars na pia kuwa mtangazaji katika shoo yakucheza 'Sakata' inayofanyika Kenya ni kwasababu kwasasa muziki kwake ni kazi.
“Muziki ni kazi kama ilivyo kazi zingine, msanii wa kike inabidi uwe na watu wa kukusimamia na uwe  makini na unachokifanya ili uweze kufanya vizuri”, Shaa.
Msani Shaa akiwa na Msanii wa Uganda Jackie , Coke Studio mwaka jana ambako msanii huyo alipata nafasi ya kuimba pamoja na wasanii wakubwa wa Africa kama Burna Boy,Chidma na nje ya Africa Wyclife Jean.


MANWATER AZUNGUMZA KUHUSU PESA WANAZOLIPWA NA WASANII

Mtayarishaji wa muziki kutoka studio za Combination Sound Manwater amesema waliyonayo maproduza wengi hapa Tanzania halingani kabisa na kazi wanazofanya.Produza huyo  anasifika kwa kutengeneza nyimbo kama Mwana ya Alikiba, Nani kama Mama ya Christian Bella,Tupogo remix ya Ommy Dimpoz na nyingine nyingi.
Manwater anasema kipato anachokipata hakiendani hata kidogo na kipato anachokipata msanii kupitia wimbo huo huo ambao produza ameutengeneza.Alieleza kuwa hii inatokana na njia ya malipo ambayo inatumika Tanzania msanii anapoenda kurekodi wimbo studio.
“Msanii anakuja ananilipa mimi laki 5 au milioni 1 wimbo unaisha anaenda kufanya shoo analipwa milioni 5, na anaendelea kufanya shoo nyingi kwa wimbo huo huo aliokulipa milioni  moja.Hii ndo maana maproduza hatuna mafanikio, sisemi hivi kwasababu nina wivu ila nataka na sisi maproduza mchango wetu katika muziki uthaminiwe”, alisema Manwater.
Produza huyo anasema yeye kwasasa anachaji shilingi milioni 1 kwa wimbo mmoja lakini kiasi hicho cha pesa kinaweza kuongeza kwasababu yeye anajiamini na anafikiria kuweka mfumo ambao utalingana na kiwango cha akili yake anachokitumia kutemtengenezea msanii wimbo.

SABABU ILIYOPELEKEA MSANII JAFARAI KUTOKUSIKIKA KWENYE MUZIKI KWA ZAIDI YA MWAKA MMOJA

Msanii Jafarai akiwa kwenye Carwash yake
Msanii wa muziki wa bongofleva Jaffary Msham maarufu kama Jafarai amesema kuwa biashara yake yakuosha magari inalipa ndo maana ameendelea kufanya biashara hiyo kwa miaka miwili sasa.
Jafarai alisema kama biashara hiyo ingekuwa haimlipi asingeweza kuendelea kuifanya, “siwezi kulalamika biashara ni nzuri hii ndo maana sijafunga mpaka leo”.Aliendelea kueleza kuwa kwasiku biashara ikiwa mbaya anaosha magari 10 mpaka 20 ambayo makadirio yake ni sawa na shilingi laki 1 na nusu mpaka 2.Kwasiku ambayo baishara ni nzuri huosha magari mpaka 30 ambayo makadirio yake ni sawa na shilingi laki nne.
Wasanii na wadau wa burudani walioenda kuosha Jafarai Carwash
Msanii huyo anasema kuwa pia biashara hiyo inaendelea kumweka karibu na mashabiki wake kwasababu wakija kuosha gari katika carwash yake wanapata nafasi yakupiga nae picha na kuongea nae.
Biashara hiyo imempelekea Jafarai aliyetamba na nyimbo kama ‘Niko Bize’, ‘Toa hela’ kuwa kimya kwenye muziki bila kutoa nyimbo takribani mwaka mmoja na nusu sasa.Jafarai anasema ni kweli amekuwa bize na biashara lakini wapenzi wake muziki watarajie wimbo mpya kutoka kwake sikuhizi za hivi karibuni.Wimbo wa mwisho ambao msanii huyo kutoa ulikuwa ni ‘Blaa Blaa’ aliokuwa amemshirikisha marehemu Ngwair.