Wednesday, November 14, 2012

MAZISHI YA MSANII WA MUZIKI WA TAARABU WA KIKUNDI CHA TOT MARIAM KHASIM YALIVYOKUWA

Baadhi ya Wasanii,Ndugu,na wapenzi wa muziki wa Taarab hapa nchini wamejumuika pamoja katika safari ya kupumzisha mwili wa aliyekuwa msanii wa kundi la TOT  marehemu Mariam Khasim katika nyumba yake ya milele.Maria Khasim alifariki wakati akijifungua Muhimbili na mtoto kutoka salama.Baadhi ya wasanii walikuwepo kwenye mazishi baadhi yao ni Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Mzee Yusuph na mke wake Bi Leila,Nyota Waziri, Bi Hindu na  wasanii wenzake wa kundi la TOT
Msanii nyota wa muziki wa Taarab hapa nchini Khadija Kopa mwenye kitambaa Chekundu akiwa pamoja na waombolezaji wengine
Inasemekana huyo alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa Marehemu, ni msanii mwenzake wa TOT anaitwa Mwasiti
Mwasiti akiwa na uchungu wa kumpoteza rafiki yake
Mtangazaji wa kipindi cha taarabu East Africa Radio Mwamfuo akiwa na mtangazaji wa Capital Radio Hawa
Waombolezaji
Isha Mishuzi
Mzee Yusuph akiwa na mke wake Bi Leila na waombolezaji wengine
Mtangazaji wa Taarabu wa Times Fm
Msanii Nyota Waziri naye alikuwepo
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mariam likiingia
Mariam Khasim kwenye picha chini, amezikwa katika makaburi ya Magomeni Makuti ameacha watoto wawili, akiwemo huyo mchanga.Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema.

1 comments:

Dah! inasikitisha sana kwakweli na Mungu amlaze mahala pema peponi amina.

Post a Comment